Trickling Out? Somo la shughuli za biashara za ikolojia/jamii katika Kusini na Mashariki mwa Afrika na jukumu lao ustawi endelevu katika msingi wa piramidi

Imedhaminiwa na ESRC Utaratibu wa Kwanza ya Ridhia

Kuanzia tarehe: 1 Februari 2011

Urefu: miezi 26

Maelezo

Lengo la msingi la somo hili ni: (a) kutambua mifano ya shughuli za biashara za jamii na za mazingira katika eneo la Ustawi wa Afrika Kusini na Jumuiya Afrika Mashariki; na (b) Kuchunguza na kutathmini majukumu ya shughuli hizi za biashara zinaweza kuchangia kama utaratibu wa 'Trickle Out' manufaa ya kijamii, kimazingira na kiuchumi kutoka katika makundi ya jumuiya yanayozingatiwa kuwa katika hali ya kiuchumi ya 'msingi/chini ya piramidi' (BOP).

Kutumia uchanganuzi wa pili wa data ya hati zilizochapishwa na wahusika kuu wa majadiliano, 'Saraka ya Shughuli za Biashara Ikolojia/Jamii, Wakala na mashirika' inakuzwa. Kutumia mchanganyiko wa methodolojia kuchanganya uchanganuzi wa nyaraka za data, ukaguzi na mahojiano na shughuli za biashara na mawakala waliotambulishwa kwa Saraka hii somo linazingatia mambo mengo ya shughuli za ustawi wa biashara za ikolojia-jamii, majukumu ya ugavi duniani kote na mashirika ya msaada na uwezekano wa athari za 'Trickle Out' za shughuli za biashara kama hizo katika jumuiya yao.

Hii inatuatia uchanganuzi stahilifu wa kina ya mifano ya kesi 9 – 12 kutoka Kenya, afrika Kusini, na Zambia ambayo inazingatia maingiliano ya shughuli hizi za biashara pamoja na mashirika ya usambazaji nchini na kote duniani, na kutathmini jukumu mahsusi ambayo shughuli kama hizo za biashara zinachangia kwa kupunguza umaskini na ustawi endelevu.

Malengo

i. Kutambua, kusanisi, na kufanyiza fasihi tangulizi inayozingatia majukumu ya shughuli za biashara za jamii na kimazingiza kufanya kupunguza umasikini na ustawi endelevu.

ii. Kukusanya saraka ya shughuli za biashara za jamii au mazingira ambazo zinazalisha, uchuuzi, kutengeneza au kutoa huduma eneo la Jumuiya ya Kustawi ya Afrika Kusini (SADC) na maeneo ya Jumuiya za Mashariki mwa Afrika, hali kadhalika mawakala ya kutoa misaada, mashirika ya hiari na mipango ya bima inayosaidia hizi.

iii.Kutathmini shughuli hizi za biashara kupitia ukaguzi na utafiti wa uchunguzi kifani ku:

  • Kupima, ramana na kuchanganua tabia zao;
  • Kutambua matokeo ya utatu ya chini katika uchumi, mazingira, na masharti ya jamii;
  • Kutambua majukumu yao katika uanzishaji wa uenezaji mfululizo wa kijani.

d) Zingatia kama matokeo ya uzidishaji inatokea kueneza uzalishaji wa fedha, jamii na binadamu katika jumuiya ya mtaanii kwa njia ya 'Trickle Out'; na

e) Kuchunguza majukumu mahsusi mashirika haya yanachangia katika kupunguza umaskini na ustawi endelevu.

Rejea juu

 

Tunakofanya kazi

Mradi wa Trickle Out inachunguza sekta za shughuli za biashara za jamii na mazingira kwa nchi 19 katika Mashariki na Kusini mwa Afrika, nchi hizi ni: Angola, Botswana, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Kenya, Lesotho, Madagaska, Malawi, Morisi, Mozambique, Namibia, Rwanda, Shelisheli, Afrika Kusini, Swaziland, Tanzania, Uganda, Zambia, Zimbabwe.

Rejea juu

 

Uchunguzi Kifani

Kama sehemu ya utafiti wa mradi wa Trickle Out tutafanya utafiti wa case stusy wa kina pamoja na shughuli za biadhara za jamii na/au jamii zilizoko Afrika Kusini, Zambia na Kenya. Shughuli za biashara za uchunguzi kifani hizi zitaonyeshwa katika tovuti hii

Tunatarajia kutekeleza kwa kina utafiti wa uchunguzi kifani na kwa sasa tunatafuta shughuli za biashara za jamii na mazingira katika nchi hizi zilizo na nia kushirikiana na mradi. Kama ungependa kushiriki kwa utafiti wetu na kuonekana kama shughuli za biashara za uchunguzi kifani tafadhali wasiliana nasi kupitia ukurasa wa wasiliana nasi.

Reja juu

 

Sisi ni akina nani

Tafadhali, bonyeza viunganishi vifuatavyo ili kujua mengi kutuhusu.

Rejea juu

Sheffield Management School

Leeds Building